2 Maana yatakupa wingi wa siku,maisha marefu na fanaka kwa wingi.
3 Utii na uaminifu visitengane nawe.Vifunge shingoni mwako;viandike moyoni mwako.
4 Hivyo utakubalika na kusifika,mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.
5 Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote,wala usitegemee akili zako mwenyewe.
6 Umtambue Mungu katika kila ufanyalo,naye atazinyosha njia zako.
7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.
8 Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako,na kiburudisho mifupani mwako.