24 Ukiketi hutakuwa na hofu;ukilala utapata usingizi mtamu.
25 Usiogope juu ya tishio la ghafla,wala shambulio kutoka kwa waovu,
26 Maana Mwenyezi-Mungu ndiye atakayekutegemeza;atakuepusha usije ukanaswa mtegoni.
27 Usimnyime mtu anayehitaji msaada,ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo.
28 Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho,hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.
29 Usipange maovu dhidi ya jirani yako,anayeishi karibu nawe bila wasiwasi.
30 Usigombane na mtu bila sababuikiwa hajakudhuru kwa lolote.