32 Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu.
33 Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu,lakini huyabariki makao ya waadilifu.
34 Yeye huwadharau wenye dharau,lakini huwafadhili wanyenyekevu.
35 Wenye hekima watavuna heshima,lakini wapumbavu watapata fedheha.