6 Umtambue Mungu katika kila ufanyalo,naye atazinyosha njia zako.
7 Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu.
8 Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako,na kiburudisho mifupani mwako.
9 Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako,na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10 Hapo ghala zako zitajaa nafaka,na mapipa yako yatafurika divai mpya.
11 Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu,wala usiudhike kwa maonyo yake;
12 maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye,kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi.