7 wanywe na kusahau umaskini wao,wasikumbuke tena taabu yao.
8 Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu;na kutetea haki za wote wasiojiweza.
9 Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki,linda haki za maskini na fukara.
10 Mke mwema kweli, apatikana wapi?Huyo ana thamani kuliko johari!
11 Mumewe humwamini kwa moyo,kwake atapata faida daima.
12 Kamwe hamtendei mumewe mabaya,bali humtendea mema maisha yake yote.
13 Hutafuta sufu na kitani,na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii.