20 Mwanangu, ya nini kutekwa na mwanamke mwasherati?Ya nini kumkumbatia kifuani mwanamke mgeni?
21 Kumbuka njia za mtu zi wazi mbele ya Mwenyezi-Mungu;yeye anaona kila hatua anayochukua binadamu.
22 Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wake mwenyewe;hukamatwa katika tanzi za dhambi yake mwenyewe.
23 Yeye hufa kwa utovu wa nidhamu,huangamia kwa sababu ya upuuzi wake mkuu.