1 Mwanangu, kama umejitolea kumdhamini jirani yako,ikiwa umetoa ahadi yako kwa ajili ya mtu huyo,
2 umejibana kwa maneno yako mwenyewe,umejinasa kwa ahadi uliyofanya.
3 Ujue kwamba uko chini ya mamlaka ya mwenzio,lakini mwanangu, ukitaka kujiokoa, basi fanya hivi:Mwendee mtu huyo mara moja umsihi akupe uhuru wako.
4 Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi,wala kope za macho yako zisinzie.
5 Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.