27 Je, waweza kuweka moto kifuanina nguo zako zisiungue?
28 Je, waweza kukanyaga makaa ya motona nyayo zako zisiungue?
29 Ndivyo alivyo mwanamume alalaye na mke wa mwenzake;yeyote anayemgusa mwanamke huyo hataacha kuadhibiwa.
30 Watu hawambezi sana mtu akiiba kwa sababu ya njaa;
31 lakini akipatikana lazima alipe mara saba;tena atatoa mali yote aliyo nayo.
32 Mwanamume anayezini na mke wa mtu hana akili kabisa;huyo hujiangamiza yeye mwenyewe.
33 Atapata majeraha na madharau;fedheha atakayopata haitamtoka.