4 Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi,wala kope za macho yako zisinzie.
5 Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo,mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji.
6 Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi,fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima.
7 Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala;
8 lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi,hujikusanyia akiba wakati wa mavuno.
9 Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini?Utaamka lini katika usingizi wako?
10 Wasema: “Acha nilale kidogo tu,acha nisinzie kidogo!Niache nikunje mikono nipumzike kidogo!”