13 Mwanamke mpumbavu ana kelele,hajui kitu wala hana haya.
14 Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake,huweka kiti chake mahali pa juu mjini,
15 na kuwaita watu wapitao njiani,watu wanaokwenda kwenye shughuli zao:
16 “Yeyote aliye mjinga na aje hapa!”Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:
17 “Maji ya wizi ni matamu sana;mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana.”
18 Lakini mjinga hajui kwamba humo mna wafu,wageni wa mwanamke huyo wamo chini Kuzimu.