7 Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi,amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa.
8 Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia;mwonye mwenye hekima naye atakupenda.
9 Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima;mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.
10 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima;na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili.
11 Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa;utaongezewa miaka mingi maishani mwako.
12 Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe;kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara.
13 Mwanamke mpumbavu ana kelele,hajui kitu wala hana haya.