3 Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu,Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia.Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba;mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.
4 Huikaripia bahari na kuikausha,yeye huikausha mito yote.Mbuga za Bashani na mlima Karmeli hunyauka,maua ya Lebanoni hudhoofika.
5 Milima hutetemeka mbele yake,navyo vilima huyeyuka;dunia hutetemeka mbele yake,ulimwengu na vyote vilivyomo.
6 Nani awezaye kuikabili ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu?Nani awezaye kustahimili ukali wa hasira yake?Yeye huimwaga hasira yake iwakayo kama moto,hata miamba huipasua vipandevipande.
7 Mwenyezi-Mungu ni mwema,yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu.Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.
8 Adui wakiivamia nchi kama mafuriko, yeye huwaangamiza;huwafuatia na kuwafukuza mpaka gizani.
9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu?Yeye atawakomesha na kuwaangamiza,wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.