6 Nani awezaye kuikabili ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu?Nani awezaye kustahimili ukali wa hasira yake?Yeye huimwaga hasira yake iwakayo kama moto,hata miamba huipasua vipandevipande.
7 Mwenyezi-Mungu ni mwema,yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu.Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.
8 Adui wakiivamia nchi kama mafuriko, yeye huwaangamiza;huwafuatia na kuwafukuza mpaka gizani.
9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu?Yeye atawakomesha na kuwaangamiza,wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.
10 Watateketezwa kama kichaka cha miiba,kama vile nyasi zilizokauka.
11 Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungualiyefanya njama za ulaghai.
12 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake:“Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu,wao wataangushwa na kuangamizwa.Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu,sitawateseni tena zaidi.