3 Na katika miji mingine, watu wa Israeli, makuhani, Walawi, walinzi wa malango na wazawa wa watumishi wa Solomoni, walikaa katika maeneo yao wenyewe, katika miji yao.
4 Baadhi ya watu wa kabila la Yuda na wa kabila la Benyamini walikaa katika mji wa Yerusalemu. Wafuatao ndio watu wa ukoo wa Yuda waliokaa mjini Yerusalemu: Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli. Wote hao ni wazawa wa Peresi.
5 Pia Maaseya, mwana wa Baruku, mwana wa Kolhoze, mwana wa Hazaya, mwana wa Adaya, mwana wa Yoyaribu, mwana wa Zekaria, Mshilo.
6 Wazawa wote wa Peresi waliokaa mjini Yerusalemu walikuwa wanaume mashujaa 468.
7 Watu wa ukoo wa Benyamini waliokaa mjini Yerusalemu ni: Salu, mwana wa Meshulamu, mwana wa Yoedi, mwana wa Pedaya, mwana wa Kolaya, mwana wa Maaseya, mwana wa Ithieli na mwana wa Yeshaya.
8 Baada ya huyo walikuwako Gabai na Salai. Jumla yao 928.
9 Yoeli, mwana wa Zikri, alikuwa ndiye mkuu wao; naye Yuda mwana wa Hasenua alikuwa mkuu wa pili wa mji.