18 wa Bilga, Shamua; wa Shemaya, Yehonathani;
19 wa Yoaribu, Matenai; wa Yedaya, Uzi;
20 wa Salai, Kalai; wa Amoki, Eberi;
21 wa Hilkia, Heshabia; na wa ukoo wa Yedaya, Nethaneli.
22 Wakati wa Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua wakuu wa jamaa za Walawi, waliorodheshwa; vilevile wakati wa utawala wa mfalme Dario wakuu wa jamaa za makuhani waliorodheshwa.
23 Wakuu wa jamaa za ukoo wa Lawi waliorodheshwa katika kitabu cha Kumbukumbu mpaka wakati wa Yohanani mjukuu wa Eliashibu.
24 Viongozi wa Walawi: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli walisimama mkabala na ndugu zao; walipangwa kuimba nyimbo za kusifu na kushukuru, kufuatana na amri ya mfalme Daudi, mtu wa Mungu.