1 Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amenia, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa mfalme Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda:
2 Mwenyezi-Mungu asema:“Nitavifagilia mbali viumbe vyote duniani:
3 Wanadamu, wanyama, ndege wa anganina samaki wa baharini;vyote nitaviangamiza.Waovu nitawaangamiza kabisa;wanadamu nitawafagilia mbali duniani.
4 Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda,kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu.Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii,na hakuna atakayetambua jina lao.
5 Nitawaangamiza wote wanaosujudu juu ya paa,wakiabudu jeshi la mbinguni.Nitawaangamiza wale wanaoniabuduna kuapa kwa jina langu,hali wanaapa pia kwa jina la mungu Milkomu.