21 Muwe macho. Wasichana wa Shilo watakapotoka nje kucheza wakati wa sikukuu, tokeni kwenye mizabibu na kila mtu ajinyakulie msichana mmoja awe mkewe. Kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.
22 Baba zao au kaka zao wakija kutulalamikia tutawaambia, “Sisi tunawaombeni mwahurumie watu wa Benyamini na kuwaachia wawachukue hao wanawake; maana hatukuwapata katika vita vya Yabesh-gileadi. Na kwa vile nyinyi wenyewe hamkutupatia hao binti zenu, hamtahukumiwa.”
23 Wale wanaume wa kabila la Benyamini wakafanya hivyo, kila mmoja akajichagulia msichana miongoni mwa wasichana waliotoka nje kucheza huko Shilo na kumchukua kuwa mkewe. Kisha wakarudi katika eneo lao, wakaijenga miji yao upya na kuishi humo.
24 Wakati huohuo Waisraeli wakaondoka, kila mtu akarudi katika eneo la kabila lake na jamaa yake. Kila mtu alirudi katika sehemu aliyogawiwa.
25 Siku hizo hapakuwepo na mfalme katika Israeli. Kila mtu alifanya kama alivyoona kuwa sawa.