1 Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,
2 “Waamuru watu wa Israeli wakuletee mafuta safi kwa ajili ya taa ili taa hiyo iendelee kuwaka daima.
3 Aroni ataiweka taa hiyo ndani ya hema la mkutano, nje ya pazia la sanduku la maamuzi ili ipate kuwaka mbele yangu tangu usiku mpaka asubuhi. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu.
4 Ataziweka hizo taa katika kinara cha taa cha dhahabu safi ziwake daima mbele ya Mwenyezi-Mungu.
5 “Chukua unga laini, kilo kumi na mbili na kuoka mikate kumi na miwili.