28 “Kisha hapo baadayenitaimimina roho yangu juu ya binadamu wote.Watoto wenu wa kike na wa kiume watatabiri,wazee wenu wataota ndoto,na vijana wenu wataona maono.
29 Hata juu ya watumishi wa kiume na wa kike,nitaimimina roho yangu wakati huo.
30 “Nitatoa ishara mbinguni na duniani;kutakuwa na damu, moto na minara ya moshi.
31 Jua litatiwa giza,na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,kabla ya kufika siku ya Mwenyezi-Mungu,siku iliyo kuu na ya kutisha.
32 Hapo watu wote watakaoomba kwa jina la Mwenyezi-Mungu wataokolewa.Maana katika mlima Siyoni na Yerusalemu,watakuwako watu watakaosalimika,kama nilivyosema mimi Mwenyezi-Mungu.