14 Wanafika makundi kwa makundikwenye bonde la Hukumu,maana siku ya Mwenyezi-Mungu imekaribia.
15 Jua na mwezi vinatiwa giza,na nyota zimeacha kuangaza.
16 Mwenyezi-Mungu ananguruma huko Siyoni;sauti yake inavuma kutoka Yerusalemu;mbingu na dunia vinatetemeka.Lakini Mwenyezi-Mungu ni kimbilio la watu wake,ni ngome ya usalama kwa Waisraeli.
17 “Hapo, ewe Israeli,utajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,nakaa Siyoni, mlima wangu mtakatifu,Yerusalemu utakuwa mji mtakatifu;na wageni hawatapita tena humo.
18 “Wakati huo, milima itatiririka divai mpya,na vilima vitatiririka maziwa.Vijito vyote vya Yuda vitajaa maji;chemchemi itatokea nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu,na kulinywesha bonde la Shitimu.
19 “Misri itakuwa mahame,Edomu itakuwa jangwa tupu,kwa sababu waliwashambulia watu wa Yudawakawaua watu wasio na hatia.
20 Bali Yuda itakaliwa milele,na Yerusalemu kizazi hata kizazi.