13 Lakini Yeroboamu aliwazungushia waviziao kwa nyuma; basi wao wakawa mbele ya Yuda, na wale waviziao nyuma yao.
14 Na Yuda walipotazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia BWANA, na makuhani wakapiga mapanda.
15 Ndipo wakapiga kelele watu wa Yuda; ikawa, watu na Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.
16 Wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao.
17 Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli mia tano elfu, watu wateule.
18 Ndivyo walivyotiishwa wana wa Israeli wakati ule, wakashinda wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea BWANA, Mungu wa baba zao.
19 Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang’anya miji, Betheli na miji yake, na Yeshana na miji yake, na Efroni na miji yake.