26 Akanyosha mkono wake akashika kigingi,Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi;Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake.Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake.
27 Miguuni pake aliinama, akaanguka, akalala.Miguuni pake aliinama, akaanguka.Hapo alipoinama, ndipo alipoanguka amekufa.
28 Alichungulia dirishani, akalia,Mama yake Sisera alilia dirishani;Mbona gari lake linakawia kufika?Mbona gurudumu za gari lake zinakawia?
29 Mabibi yake wenye akili wakamjibu,Naam, alijipa nafsi yake jawabu.
30 Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya,Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu?Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbali mbali,Nyara za mavazi ya rangi mbali mbali ya darizi;Ya rangi mbali mbali ya darizi, pande zote mbili,Juu ya shingo za hao mateka.
31 Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA.Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arobaini.