10 Hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu akayapiga makofi; Balaki akamwambia Balaamu, Nalikuita ili unilaanie adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa mara tatu hizi.
11 Basi sasa kimbilia mahali pako; naliazimu kukuheshimu sana; lakini, tazama, BWANA amekuzuilia heshima.
12 Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionipelekea, nikisema,
13 Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.
14 Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho.
15 Akatunga mithali yake akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema,
16 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu.Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,