1 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma maragoni, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya wafu;
3 mtawatoa nje wote, waume kwa wake, mtawaweka nje ya marago; ili wasiyatie unajisi marago yao, ambayo mimi naketi katikati yake.
4 Wana wa Israeli wakafanya vivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya marago; kama BWANA alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
5 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
6 Uwaambie wana wa Israeli, Mtu mume au mke atakapofanya dhambi yo yote, ifanywayo na binadamu, kumwasi BWANA, na mtu huyo akawa na hatia;
7 ndipo watakapoungama dhambi yao waliyoifanya; naye atarudisha kwa hatia yake, kwa utimilifu wake, tena ataongeza juu yake sehemu ya tano, na kumpa huyo aliyemkosa.