41 Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya BWANA, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na BWANA. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani.
42 BWANA akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu.
43 Basi niliwaambia, msinisikize, bali mliasi amri ya BWANA, mkajikinai, na kukwea mlimani.
44 Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki, wakawapomoshea Seiri mpaka Horma.
45 Mkarudi mkalia mbele za BWANA; BWANA asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.
46 Ndipo mkakaa Kadeshi siku nyingi, kwa kadiri ya hizo siku mlizokaa.