13 Sasa basi ondokeni, mkakivuke kijito cha Zeredi. Nasi tukakivuka kile kijito cha Zeredi.
14 Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, zilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya marago, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na BWANA.
15 Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa kati ya marago, hata walipokoma.
16 Basi ikawa, walipokwisha angamizwa kwa kufa watu wote wa vita kati ya watu,
17 BWANA aliniambia, akasema,
18 Hivi leo ivuke Ari, mpaka wa Moabu;
19 na utakaposongea kuwaelekea wana wa Amoni, usiwasumbue wana wa Amoni, wala usishindane nao; kwa kuwa sitakupa katika nchi ya hao wana wa Amoni kuwa milki yako; kwa sababu nimewapa wana wa Lutu iwe milki yao.