5 Na huko umjengee madhabahu BWANA, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.
6 Jenga hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee BWANA, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;
7 ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako.
8 Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana.
9 Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako.
10 Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo.
11 Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema,