10 Alimkuta katika nchi ya ukame,Na katika jangwa tupu litishalo;Alimzunguka, akamtunza;Akamhifadhi kama mboni ya jicho;
11 Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake;Na kupapatika juu ya makinda yake,Alikunjua mbawa zake, akawatwaa,Akawachukua juu ya mbawa zake;
12 BWANA peke yake alimwongoza,Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.
13 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka,Naye akala mazao ya mashamba;Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini,Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;
14 Siagi ya ng’ombe, na maziwa ya kondoo,Pamoja na mafuta ya wana-kondoo,Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi,Na unono wa ngano iliyo nzuri;Ukanywa divai, damu ya mizabibu.
15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke;Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda;Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya,Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni,Wakamkasirisha kwa machukizo.