12 BWANA peke yake alimwongoza,Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.
13 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka,Naye akala mazao ya mashamba;Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini,Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;
14 Siagi ya ng’ombe, na maziwa ya kondoo,Pamoja na mafuta ya wana-kondoo,Kondoo waume wa Kibashani, na mbuzi,Na unono wa ngano iliyo nzuri;Ukanywa divai, damu ya mizabibu.
15 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke;Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda;Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya,Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
16 Wakamtia wivu kwa miungu migeni,Wakamkasirisha kwa machukizo.
17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu,Kwa miungu wasiyoijua,Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu,Ambayo baba zenu hawakuiogopa.
18 Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa,Mungu aliyekuzaa umemsahau.