16 Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake,Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti;Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu,Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.
17 Mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wake mume, enzi ni yake;Na pembe zake ni pembe za nyati;Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi;Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu,Nao ni maelfu ya Manase.
18 Na Zabuloni akamnena,Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako;Na Isakari, katika hema zako.
19 Watayaita mataifa waje mlimani;Wakasongeze huko sadaka za haki;Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari,Na akiba zilizofichamana za mchangani.
20 Na Gadi akamnena,Na abarikiwe amwongezaye Gadi;Yeye hukaa kama simba mke,Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
21 Akajichagulia sehemu ya kwanza,Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;Akaja pamoja na wakuu wa watu,Akaitekeleza haki ya BWANA,Na hukumu zake kwa Israeli.
22 Na Dani akamnena,Dani ni mwana-simba,Arukaye kutoka Bashani.