5 Simeoni na Lawi ni ndugu;Panga zao ni silaha za jeuri.
6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao,Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao,Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu,Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe;
7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali,Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.Nitawagawa katika Yakobo,Nitawatawanya katika Israeli.
8 Yuda, ndugu zako watakusifu,Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako.Wana wa baba yako watakuinamia.
9 Yuda ni mwana-simba,Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda;Aliinama akajilaza kama simba,Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda,Wala mfanya sheria kati ya miguu yake,Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki,Ambaye mataifa watamtii.
11 Atafunga punda wake katika mzabibu,Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri.Amefua nguo zake kwa mvinyo,Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.