1 Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa,Huo uliokuwa umejaa watu!Jinsi alivyokuwa kama mjane,Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa!Binti mfalme kati ya majimbo,Jinsi alivyoshikwa shokoa!
2 Hulia sana wakati wa usiku,Na machozi yake yapo mashavuni;Miongoni mwa wote waliompendaHakuna hata mmoja amfarijiye;Rafiki zake wote wamemtenda hila,Wamekuwa adui zake.
3 Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa,Na kwa sababu ya utumwa mkuu;Anakaa kati ya makafiri,Haoni raha iwayo yote;Wote waliomfuata wamempataKatika dhiki yake.
4 Njia za Sayuni zaomboleza,Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu;Malango yake yote yamekuwa ukiwa,Makuhani wake hupiga kite;Wanawali wake wanahuzunika;Na yeye mwenyewe huona uchungu.
5 Watesi wake wamekuwa kichwa,Adui zake hufanikiwa;Kwa kuwa BWANA amemtesaKwa sababu ya wingi wa makosa yake;Watoto wake wadogo wamechukuliwa matekaMbele yake huyo mtesi.