19 Naliwaita hao walionipendaLakini walinidanganya;Makuhani wangu na wazee wanguWalifariki mjini;Hapo walipokuwa wakitafuta chakulaili kuzihuisha nafsi zao.
20 Angalia, Ee BWANA; maana mimi ni katika dhiki;Mtima wangu umetaabika;Moyo wangu umegeuka ndani yangu;Maana nimeasi vibaya sana;Huko nje upanga hufisha watu;Nyumbani mna kama mauti.
21 Wamesikia kwamba napiga kite;Hakuna hata mmoja wa kunifariji;Adui zangu wote wamesikia habari ya mashaka yaliyonipata;Hufurahi kwa kuwa umeyafanya hayo;Utaileta siku ile uliyoitangaza,Nao watakuwa kama mimi.
22 Huo uovu wao woteNa uje mbele zako wewe;Ukawatende wao kama ulivyonitenda mimiKwa dhambi zangu zote;Kwa maana mauguzi yangu ni mengi sana,Na moyo wangu umezimia.