14 Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.
15 Sikilizeni ninyi, kategeni masikio yenu; msifanye kiburi; maana BWANA amenena.
16 Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
17 Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa hali ya kufungwa.
18 Mwambie mfalme, na mama ya mfalme,Nyenyekeeni na kuketi chini;Kwa maana vilemba vyenu vimeshuka,naam, taji ya utukufu wenu.
19 Miji ya Negebu imefungwa malango yake,wala hapana mtu wa kuyafungua;Yuda amechukuliwa hali ya kufungwa;amechukuliwa kabisa hali ya kufungwa.
20 Inua macho yako, Ee Yerusalemu, ukawatazame hawa wanaokuja kutoka kaskazini; liko wapi kundi lako ulilopewa, kundi lile zuri?