2 Basi nikanunua mshipi sawasawa na neno la BWANA, nikajivika viunoni.
3 Nalo neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema,
4 Twaa mshipi ule ulioununua, ulio viunoni mwako, kisha ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukaufiche huko katika pango la jabali.
5 Basi nikaenda, nikauficha karibu na mto Frati, kama BWANA alivyoniamuru.
6 Hata ikawa, baada ya siku nyingi, BWANA akaniambia, Ondoka, enenda mpaka mto Frati, ukautwae ule mshipi, niliokuamuru kuuficha huko.
7 Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikautwaa ule mshipi katika mahali pale nilipouficha; na tazama, mshipi ulikuwa umeharibika, haukufaa tena kwa lo lote.
8 Ndipo neno la BWANA likanijia, kusema,