7 Nami nitakufanyia tayari watu wenye kuharibu,kila mtu na silaha zake;Nao watakata mierezi miteule yako,na kuitupa motoni.
8 Na mataifa mengi watapita karibu na mji huu, nao watasema kila mtu na jirani yake, Nini maana yake BWANA kuutenda hivi mji huu mkubwa?
9 Ndipo watakapojibu, Ni kwa sababu waliliacha agano la BWANA, Mungu wao, wakaabudu miungu mingine, na kuitumikia.
10 Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee,Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali;Kwa maana yeye hatarudi tena,Wala hataiona nchi aliyozaliwa.
11 Maana BWANA asema hivi, katika habari za Shalumu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; aliyemiliki badala ya Yosia, baba yake, yeye aliyetoka mahali hapa; Hatarudi huku tena;
12 bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe.
13 Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu!Na vyumba vyake kwa udhalimu!Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira,Wala hampi mshahara wake;