1 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema,
2 BWANA Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia.
3 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema BWANA; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.
4 Na haya ndiyo maneno aliyosema BWANA, katika habari za Israeli, na katika habari za Yuda.
5 Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.
6 Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona utungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi.
7 Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.