21 Niione bendera hata lini, na kuisikia sauti ya tarumbeta?
22 Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.
23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.
24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko.
25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.
26 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za BWANA, na mbele za hasira yake kali.
27 Maana BWANA asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini sitaikomesha kabisa.