2 Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakaposikizisha mshindo wa vita juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema BWANA.
3 Piga yowe, Ee Heshboni,Kwa maana Ai umeangamizwa;Lieni, enyi binti za Raba,Mjivike nguo za magunia;Ombolezeni, mkipiga mbioHuko na huko kati ya maboma;Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa,Makuhani wake na wakuu wake pamoja.
4 Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijilia?
5 Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, BWANA wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao.
6 Lakini baada ya hayo nitawarudisha wana wa Amoni walio utumwani, asema BWANA.
7 Habari za Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hapana tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?
8 Kimbieni, rudini nyuma, kaeni chini sana, enyi mnaokaa Dedani; maana nitaleta msiba wa Esau juu yake, wakati nitakapomwangalia.