21 Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao;Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu.
22 Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wake.
23 Habari za Dameski.Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia;Maana wamesikia habari mbaya;Wameyeyuka kabisa;Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.
24 Dameski umedhoofika;Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika;Dhiki na huzuni zimeupata,Kama za mwanamke katika utungu wake.
25 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu?
26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi.
27 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.