23 Habari za Dameski.Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia;Maana wamesikia habari mbaya;Wameyeyuka kabisa;Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.
24 Dameski umedhoofika;Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika;Dhiki na huzuni zimeupata,Kama za mwanamke katika utungu wake.
25 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu?
26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA wa majeshi.
27 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi.
28 Habari za Kedari, na za falme za Hazori, ambazo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alizipiga. BWANA asema hivi, Ondokeni, pandeni hata Kedari, mkawateke nyara wana wa mashariki.
29 Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia zao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote.