17 Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa;Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga;Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo,Wala hamna pumzi ndani yake.
18 Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu;Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.
19 Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;Na Israeli ni kabila ya urithi wake;BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;
22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;
23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.