14 bali wameenenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao.
15 Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe.
16 Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa.
17 BWANA wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje;
18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni,Jinsi tulivyotekwa!tulivyofadhaika sana!Kwa sababu tumeiacha nchi,kwa kuwa wameangusha makao yetu.
20 Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake,Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake;Mkawafundishe binti zenu kuomboleza,Na kila mmoja jirani yake kulia.