18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni,Jinsi tulivyotekwa!tulivyofadhaika sana!Kwa sababu tumeiacha nchi,kwa kuwa wameangusha makao yetu.
20 Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake,Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake;Mkawafundishe binti zenu kuomboleza,Na kila mmoja jirani yake kulia.
21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu,imeingia majumbani mwetu;Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje,na vijana katika njia kuu.
22 Nena, BWANA asema hivi,Mizoga ya watu itaangukakama samadi juu ya mashamba,Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye,wala hapana mtu atakayeikusanya.
23 BWANA asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
24 bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,