13 Wakati huohuo, kukatokea tetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhi ikaharibiwa. Watu 7,000 wakauawa kwa tetemeko hilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
14 Maafa ya pili yamepita; lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima.
15 Kisha, malaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sauti kuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa ufalme wa ulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Naye atatawala milele na milele!”
16 Kisha, wale wazee ishirini na wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
17 wakisema:“Tunakushukuru ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu,uliyeko na uliyekuwako!Maana umetumia nguvu yako kuu, ukaanza kutawala!
18 Watu wa mataifa waliwaka hasira,lakini ghadhabu yako imefika,naam wakati wa kuwahukumu wafu.Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii,watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo.Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”
19 Kisha hekalu la Mungu mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana hekaluni mwake. Kukatokea umeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvua kubwa ya mawe.