42 Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani na Akani; na wana wa Dishoni walikuwa Usi na Arani.
43 Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.
44 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake.
45 Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemi alitawala badala yake.
46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu.
47 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka alitawala badala yake.
48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ulio karibu na mto Eufrate, alitawala badala yake.