24 Baada ya Hesroni kufariki, Kalebu alimwoa Efratha, mjane wa Hesroni, baba yake. Efratha alimzalia Kalebu mwana jina lake Ashuri, aliyekuwa mwanzilishi wa mji wa Tekoa.
25 Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, alikuwa na wana watano: Ramu, mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.
26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine jina lake Atara. Huyu alimzalia Yerameeli mwana, jina lake Onamu.
27 Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini na Ekeri.
28 Wana wa Onamu walikuwa Shamai na Yada. Nao wana wa Shamai walikuwa Nadabu na Abishuri.
29 Abishuri alioa mke, jina lake Abihaili, naye akamzalia wana wawili: Abani na Molidi.
30 Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu; lakini Seledi alifariki bila watoto.