21 Merari alikuwa na wana wawili: Mali na Mushi. Wana wa Mali walikuwa wawili: Eleazari na Kishi.
22 Eleazari alifariki bila kupata mtoto wa kiume, ila mabinti tu. Mabinti hao waliolewa na binamu zao, wana wa Kishi.
23 Wana wa Mushi walikuwa watatu: Mali, Ederi na Yeremothi.
24 Hao ndio wana wa Lawi kulingana na koo zao. Kila mmoja wao aliyetimiza umri wa miaka ishirini na zaidi, aliandikishwa kwa jina, na alishiriki katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
25 Daudi alisema, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, amewapa watu wake amani, naye ataishi Yerusalemu milele.
26 Kwa hiyo, Walawi hawatahitaji tena kulibeba hema takatifu au vyombo vyake vya ibada.”
27 Kulingana na maagizo ya mwisho aliyotoa Daudi, Walawi wote waliofikia umri wa miaka ishirini waliandikishwa.