4 Wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.
5 Mungu alimpa Hemani, mwonaji wa mfalme, hawa watoto wa kiume kumi na wanne, na wa kike watatu, kama alivyoahidi ili kumtukuza.
6 Wanawe wote walipiga muziki kwa matoazi, vinanda na vinubi, kwenye ibada katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakiwa chini ya uongozi wa baba yao. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya amri ya mfalme.
7 Idadi yao pamoja na wale ndugu zao Walawi waliofundishwa kumwimbia Mwenyezi-Mungu, wote waliokuwa stadi, ilikuwa 288.
8 Wote, wakubwa kwa wadogo, waalimu kwa wanafunzi, walitumia kura katika kupanga kazi zao.
9 Kura ya 1 ilimwangukia Yosefu wa jamaa ya Asafu; ya 2 Gedalia pamoja na ndugu zake na wanawe kumi na wawili;
10 ya 3 Zakuri pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili;