31 Gedori, Ahio, Zekeri,
32 na Miklothi baba yake Shimea. Hawa pia waliishi Yerusalemu karibu na watu wengine wa ukoo wao.
33 Neri alimzaa Kishi, Kishi akamzaa Shauli. Shauli alikuwa na wana wanne: Yonathani, Malki-shua, Abinadabu na Eshbaali.
34 Yonathani alimzaa Merib-baali, na Merib-baali akamzaa Mika.
35 Mika alikuwa na wana wanne: Pithoni, Meleki, Terea na Ahazi.
36 Ahazi alimzaa Yehoada. Naye Yehoada aliwazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri. Zimri alimzaa Mosa.
37 Mosa alimzaa Binea, aliyemzaa Rafa, aliyemzaa Eleasa, naye Eleasa akamzaa Aseli.